Maid – filamu itakayonogesha wikiendi yako

HomeBurudani

Maid – filamu itakayonogesha wikiendi yako

Baada ya kupata manyanyaso kutoka kwa mzazi mwenzie aliyekuwa akimtukatana, kumpiga na hata kumrushia vitu vya hatari kama chupa, Alex anashindwa kuvumilia zaidi. Sean ambaye amekuwa akifanya manyanyaso yote hayo mbele ya binti yao aitwaye Maddy mwenye miaka miwili tu.

Alex hakuona sababu ya kuendelea na mahusiano ya vurugu kila uchao na ili kuokoa jahazi, anaamua kuondoka na mwanae tena akiwa na begi tu la nguo bila kujua ni wapi wataenda kuishi na watakula nini.

Clean Bandit hawakukosea walipoimba kibao cha Rockabye, ambacho kinaelezea jinsi ‘single mothers’ wengi wanavyopambana kwa hali na mali ili kuwalea watoto wao, kwa Alex pia ilikuwa hivyo hivyo. Licha ya kuwa na umri wa miaka 23 tu, jukumu la kuwa Mama linamfanya kuwa tayari kufanya chochote ili mradi apate kipato cha kumtunza mwanaye.

Je? maisha ya tabu na huzuni ya Alex na mwanae yatapata ahueni siku moja? Jibu lipo katika filamu hii ya ‘Maid’ na ukitazama utaguswa sana na kupata picha vile ‘single mothers’ wanavyopitia magumu ili mradi tu watoto wao wapate chochote kitu.

error: Content is protected !!