Oman kujenga Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro

HomeKitaifa

Oman kujenga Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro

Hatimaye ziara ya siku tatu nchini Oman iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan imeanza kuzaa matunda baada ya Viwanja vya ndege Muscat kutia saini ya makubaliano (MoU) na Kampuni ya Maendeleo ya Viwanja vya Ndege ya Kilimanjaro (KADCO) Jumatatu ya tarehe 13 mwezi Juni mwaka huu.

Kupitia makubaliano hayo yaliyotiwa saini na Makamu wa Rais na Maendeleo ya Biashara Viwanja vya Ndege vya Oman, Mhe.Abdul Nasser Abdullah al Yamani na Christine Mwakatobe wa KADCO, Tanzania itanufaika na uzoefu wa Viwanja vya Ndege vya Oman katika usimamizi wa viwanja vya ndege huduma za VIP.

Katika makubaliano hayo, Viwanja vya Ndege vya Oman vitafanya uendelezaji wa Jengo la Watu Mashuhuri (VIP), ujenzi wa hoteli ya nyota tano kwa ajili ya abiria na jengo la biashara/maduka makubwa katika uwanja huo.

Aidha, makubaliano haya yatasaidia katika kuendeleza miundombinu iliyoainishwa katika mkataba wa MoU ili kuhakikisha kuna utoaji mzuri wa huduma za hali ya juu kama sehemu ya juhudi za kuongeza mapato kwa serikali ya Tanzania.

error: Content is protected !!