Mchumba wa Marehemu Khashoggi asikitishwa na Mwanamfalme kuinunua Newcastle

HomeMichezo

Mchumba wa Marehemu Khashoggi asikitishwa na Mwanamfalme kuinunua Newcastle

Baada ya Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia kuinunua klabu ya mpira wa miguu ya Newcastle United  inyoshiriki Ligi Kuu Uingereza, mchumba wa aliyekuwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi amesema ni jambo la kuvunja moyo wake.

Jamal Khashoggi aliuawa Oktoba 2018 alipokwenda kutembelea ubalozi wa Saud Arabia, Istanbul Uturuki. Ambapo Mwana Mfalme wa Saud Arabia alihusishwa na kifo chake kutokana na Jamal kuwa mkosoaji wa mwanamfalme huyo, ingawa Mwanamfalme alikataa tuhuma hizo.

Mpenzi huyo ya Khashoggi anayejulikana kama Hatice Cengiz amesema kipindi chote ambacho mpenzi wake hayupo yeye ameendelea kuhakikisha  anajitahidi kutafuta haki ya Jamal.

Mamlaka za soka nchini Uingereza zilizotao taarifa ya kuidhinisha kuuzwa kwa klabu ya Newcastle United baada ya kupokea hakikisho la kisheria kwamba Saudi Arabia haitaidhibiti klabu hiyo.

error: Content is protected !!