Offset amzawadia Cardi B jumba la kifahari

HomeBurudani

Offset amzawadia Cardi B jumba la kifahari

Nyota wa muziki wa “Rap” kutoka nchini Marekani Cardi B, amezawadiwa jumba la kifahari na mume wake Offset ikiwa ni zawadi kwenye siku yake ya kuzaliwa. Jumba hilo lipo katika visiwa vya Jamhuri ya Dominica (Dominican Republic)

Hii sio mara ya kwanza kwa Offset kumpa zawadi zenye thamani kubwa Mke wake ambaye wamebarikiwa kupata watoto wawili, mwaka jana ingawa walikuwa kwenye mvutako uliokaribia wawili hao kupeana talaka lakini Offset alimzawadia Cardi B gari aina ya Rolls Royce.

Wasanii na watu maarufu ambao wamehudhuria kwenye sherehe hizo za “Bithday” ya Cardi B ni Tiffany Haddish, Teyana Taylor, 2 Chainz, Lizzo, Snoop Dogg, Taraji P. Henson, Chance the Rapper, Winnie Harlow, Karrueche, PnB Rock, Anitta, Larsa Pippen, Megan Thee Stallion na  Trey Songz.

error: Content is protected !!