Sababu sita zinazoweza kumfanya mwanamke achepuke

HomeElimu

Sababu sita zinazoweza kumfanya mwanamke achepuke

Wanaume wengi wamekuwa wakijiuliza kwanini wanawake wao huwa wanachepuka ilhali huwapatia kila kitu ndani ya ndoa. Hivyo basi nakusogezea baadhi ya sababu za kuchepuka;

1.Mahusiano ya nyuma
Baadhi ya wanawake huwa na mahusiano na wanaume wengine wa zamani kabla ya kuingia kwenye ndoa, hivyo kama atakua hajaachana nao ni rahisi kwake kuchepuka nao hata akiwa ameshaolewa na mtu mwingine, wenyewe husema ‘kupasha viporo’.

2.Kulipiza kisasi
Wanawake wengine huamua kuchepuka ili kulipiza kisasi kwa mume wake baada ya kumfumania na mtu mwingine, hivyo uamua kuchukua maamuzi haya kama kumuumiza mwanaume huyo au kumuonesha kama na yeye anaweza kuchepuka.

3. Kuangalia sana video na picha za ngono.
Mwanamke anaependa kuangalia video na picha za ngono ni rahisi kwake kuchepuka kwani atataka kujaribu tendo hilo na mwanaume mwingine tofauti na mume wake wa ndoa.

  > Hatari 4 za kutoka na kimapenzi na rafiki yako

4.Umbali
Wanandoa waishio mbalimbali ni rahisi kwa mwanamke kuchepuka kama atashindwa kuvumilia upweke aliokua nao.

5.Mitandao ya kijamii
Mwanamke anaependa sana kutumia mitandao ya kijamii basi ni rahisi kwake kuchepuka kwani kwenye mitandao hiyo kuna wanaume wa aina mbalimbali na endapo anaanza mazungumzo nao basi lazima atachepuka.

6.Kuolewa kwa kulazimishwa
Kama mwanamke huyo ameolewa kwa kulazimishwa basi kuchepuka kwake ni lazima sababu atakua hampendi huyo mwanaume.

error: Content is protected !!