Hatari 4 za kutoka na kimapenzi na rafiki yako

HomeElimu

Hatari 4 za kutoka na kimapenzi na rafiki yako

 

1. Ngono inaweza kubadili kila kitu
Ngono ina tabia na kubadili vitu, na kama ukishiriki tendo la ndoa na rafiki yako kwa karibu, haina aina ya urafiki wenu hubadilika kabisa. Unapomtazama mtu ambaye ni rafiki yako tu, ni tofauti kabisa na unavyomtazama mtu ambaye umeshawahi kushiriki nae tendo la ndoa.

Kwahiyo ikitokea umeshiriki tendo na rafiki yako, hata namna unavyomtazama inabadilika kabisa. Hatari yake ni kwamba, unaweza kupoteza vitu viwili kwa muda mmoja endapo utakuwa na mahusiano na rafiki yako wa karibu. Kama mtaingia kwenye mgogoro, basi utapoteza rafiki na mpenzi, na wakati huu kurudisha mahusiano ya urafiki na mapenzi ni ngumu sana.

2. Kushindwa kusoma viashiria vibaya
Ni ngumu sana kugundua ishara mbaya (red flags) kwa wapenzi ambao walishawahi kuwa rafiki zetu, na rahisi zaidi kugundua dalili za tofauti katika mahusiano na mtu ambaye hukuwahi kumjua awali.

Kuna baadhi ya mambo rafiki yako akifanya utaona ni kawaida kwa kuwa ni rafiki yako, lakini kitu hichohicho huwezi kukubali endapo kitafanywa na mpenzi ambaye hakuwahi kuwa rafiki yako. Mara nyingi huwa tunadhani tunajua kila kitu kuhusu rafiki zetu, si kweli.

3. Historia ya rafiki yako itakutesa
Ni wazi ukiwa na rafiki wa jinsi tofauti ni lazima itakuwa ameshawahi kuwa na mtu mwingine kabla yako. Kama rafiki wa karibu, utakuwa na unajua mahusiano yake yaliyopita na unajua ni nani anampenda na unaweza kujua hisia zake pia.

Na rafiki yako anajua mambo yako pengine kama wewe unavyomjua. Hivyo basi, ni ngumu sana kuwa na mahusiano na mtu ambaye anamjua alimpenda fulani, kukabiliana na hisia hii kwa mtu unayempenda ni ngumu sana.

4. Mapenzi na urafiki ni maji na mafuta
Wapo wanaojidanganya kuwa na mahusiano ya kingono tu na rafiki zao wakiweka mipaka ya kutokuwa na mahusiano ya kudumu (friends with benefit). Ugumu unakuja pale umeshakolea na mapenzi ya rafiki yako lakini usingependa hata kidogo uwe nae katika mahusiano.

Hili ni tatizo, kwakuwa hata siku ukifanikiwa kuwa katika mahusiano mengine, kuna hatari ya kushiriki penzi na rafiki yako na kuharibu mahusiano yako ya sasa.

error: Content is protected !!