Wanaume: Fahamu meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako kudumisha penzi lako

HomeElimu

Wanaume: Fahamu meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako kudumisha penzi lako

Wanaume: Fahamu meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako kudumisha penzi lako

Maneno mazuri yana mchanago mkubwa sana katika mahusiano ya kimapenzi. Hivyo kila wakati tumia maneno mazuri ili kudumisha mapenzi yenu kwa muda mrefu.

Zifuatazo ni meseji nzuri za kumtumia mpenzi wako ili akupende daima:

  1. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.
  2. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mimi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunzie langu penzi!
  3. Kuwa nawe najivunia, mtoto mapenzi wayajua, kiuno, sauti yako tamu mithili ya chiriki wajua hasa kuitumia, mua wangu wajua kuukamua, ukiniacha jua nitaumia, nakupenda usije niacha nitajiua!
  4. Hakika nimepata tabibu, maradhi yangu wajua kuyatibu, napenda jinsi unavyonitibu, huna papara yaani ni taratibu, mpenzi usijemuonyesha mwingine hizo zako zabibu, maswahibu yakatayonisibu hakuna atakayeweza kuyatibu, nakupenda.
  5. Wangu kipenzi ninayekuenzi, jua wanitia uchizi na kuninyima usingizi, sijui kama una kizizi au ni mapenzi ndiyo yaninyima huo usingizi, la azizi nimekumiss kichizi, u hali gani mpenzi?
  6. Nimeamini wewe ni mtalam wajua kunitoa hamu, unipapasapo huhisi kupoteza fahamu, maneno yako matamu hunizidisha hamu, hakika wajua kunikamua, luv u.
  7. Giza limeingia simuoni wakunikumbatia niko kama kinda la njiwa na zaidi ya mshitakiwa mwenye hatiya, sjiui wapi joto kwa kwakulipatia na wajua kipupwe kimewadia, uko wapi my dear?
  8. Dear siku zimekaribia, miaka utatimiza katika hii dunia, hakika najivunia kupata mpenzi aliyetulia, hongera kwa wako wazazi kwa kunizalia kipenzi, zawadi yangu toka kwangu ni ahadi ya kulienzi lako penzi. Happy Birthday mpenzi.
  9. Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sina thamani katika hii dunia!
  10. Naamini utakuwa umerejea kwenye yako makazi na umechoka na kazi mpenzi, badili yako mavazi, bafuni ingia upate maji kujimwagia, nakupenda la azizi, pole sana na kazi!
error: Content is protected !!