Wanawake: Njia tano (5) za kupata pesa kiulaini kutoka kwa mwanaume

HomeElimu

Wanawake: Njia tano (5) za kupata pesa kiulaini kutoka kwa mwanaume

Utamaduni wa wanaume kuhudumia familia umekuwepo kwa miaka mingi sana duniani. Jamii nyingi duniani hasa barani Afrik a wanaume wamekuwa wakihangaikia familia zao kujipatia mahitaji mbalimbali kama chakula, mavazi, makazi mazuri na hata elimu maji na kadhalika.

Lakini kadiri siku zinavyokwenda, mahitaji yanaongezeka na maisha yanakuwa magumu, hivyo kuwafanya wanaume wengi ambao ndio watafutaji, kuwa na misimamo tofauti hasa kwenye matumizi ya fedha.

Wanawake wengi wanaripoti kuwa pochi za wanaume zimekuwa ngumu zaidi kipindi sana kipindi hiki. Hali hii kimsingi haiwafurahishi wanawake wengi, ingawa kwa walio wengi ni ngumu kukiri hilo. Ugumu wa wanaume hautokani na kutokuwa nafedha, bali uamuzi tu muda mwingine.

Clickhabari kutokana na uchunguzi wetu, tumegundua njia tano (5) ambazo kama mwanamke atazitumia, ana asilimia 95% za kupewa fedha na mwanaume/mume kama ataomba. Hapa ni kuomba jamani wasichana, sio kuiba au kutapeli au kuiba.

  1. Chakula Kitamu
    Wanaume wanapenda chakula kitamu, pindi wanapotoka kwenye mihangaiko ya kila siku basi nafsi zao husuuzika pindi wakikuta chakula kilichopikwa vizuri. Mapishi mazuri au chakula kitamu mwanamke anaweza kuitumia kama silaha katika kuombe hela kutoka kwa mume au mwanaume wake. Lakini hii lazima mwanamke ahakikishe hali chakula mpaka mume arudi ili waweze kula pamoja. Mwanaume anapokula kama chakula ni kitamu, basi ni dhahiri atasifia bila hiyana, hapo usiwe na haraka, msubiri amalize kula halafu muache apumzike kidogo, kisha penyeza shida zako ndogondogo. Kutokana na furaha aliyonayo mwanaume kutokana na chakula kitamu, kuna asimilia nyingi za yeye kukupa fedha kama anayo.
  1. Mpende mno mama yake
    Wanaume wanawapenda sana mama zao, yaani ukitaka kugombana na mwanaume na msipatane kwa namna yeyote ile onesha hata dalili ya kutompenda mama yake mzazi. Mwanamke, upendo kwa mama mkwe wako ni moja ya sihala kubwa sana katika kutengeneza upendo mkubwa kwa mume/mpenzi wako. Penda kumnunulia mama mkwe wako zawadi ndogondogo, mjulie hali hata kwa simu na mtembelee umsaidie kazi za nyumbani. Sifa nzuri zikitoka kwa mama mkwe wako kuenda kwa mume wako, ni ngumu sana mume huyo kukupuuza au kukuchuki. Umuombapo pesa mtu huyo, ana asilia kubwa sana za kukupatia kwani anadhani kwa pesa, unaweza kumjali mama yake kwa chochote.

    > Mtindo huu unaweza kusababisha uume kuvunjika wakati wa kujamiiana

  1. Kama ana mtoto, mpende sana mtoto huyo
    Hakupunguzi chochote kwa mwanamke kumpenda mtoto ambaye hujazaa na mwanaume huyo. Ukiachilia mama mzazi, wanaume huwambii kitu kuhusu watoto/mtoto wake. Ukionesha upendo wa hali ya juu kwa watoto wake kama kuwanunulia zawadi na kuwajali, basi ni kilanishi kikubwa sana cha nafsi na mifuko ya mwanaume wako. Hata kama mtoto huyo huishi nae, bali muulizie tu na mara nyingine mpe Baba yake zawadi ampelekee kwa niaba yako, hapo mwanaume huyo nikuhakikishie, akiwa nacho ukimuomba hakunyimi, na hata anaweza kukopa kwa ajili yako, siri nawapa dada na mama zangu.
  1. Usijibizane nae
    Kisanyansi kabisa na kasaikolojia, mwanaume wanasema ni ‘competitive in nature’, yaani ni kiumbe kinachoaimini kwamba kimeumbwa kushinda muda wote. Hii inamfanya mwanaume ahisi yuko juu zaidi ya wanawake muda mwingine, japo sio sawa. Na hata kipindi cha ugomvi au majibizano, mwanaume anataka yeye ndio aonekane ameshinda na yuko sawa. Hii dada zangu isikupe wasiwasi, kumkubalia yuko sawa haina maana yuko sawa, jifunze kukaa kimya au hata kuitikia anacho sema. Na wanaume wanajua kwamba kuna muda hawako sahihi, lakini kukubali ni ngumu na ni tabia yao ya asili kufanya hivyo. Chakufanya ni kukubali tu, kaa kimya, mpe ushindi akidhi kiu yake ya kutaka kuwa juu. Haikufanyi kuwa mnyonge wala mdhaifu kufanya hivyo, na wala kubishana nae na kushinda haikufanyi kuwa bora. Ukimuonesha utulivu na upole, ni rahisi kutuama nafsi yake na kukuza mapenzi juu yako.
  1. Mnunulie zawadi mwanaume wako
    Wanawake hudhani ni wao tu ndio wanapaswa kupewa muda wote, la hasha, hata wanaume wanahitaji sana mapenzi kutoka kwa wenza wao. Nafsi za wanaume kuridhishwa na vitu vidogo sana, kumununulia zawadi ndogondogo nu kuwafanya uwekezaji kwenye mfuko wa mume/mwanaume wako. Siku utakayoamua kumuomba atafikiria kwamba huwa hata wewe unamkumbuka, hivyo anakuwa hana budi kukupatia. Hebu fikiria siku zote wewe ni mtu wa kupokea tu, hata siku moja hujawahi kutoa hata kitu kidogo.

Ukweli kwamba mwanaume anapaswa kuandaa mazingira ya kushinda nafsi ya mume/mwanaume wake pindi anapoomba pesa. Hii haihitaji tu maneno makavu, bali unjanja hasa katika kuathiri saikolojia ya mwanaume. Nadhani somo limeeleweka.

error: Content is protected !!