Kufanya ngono kwa mdomo kwamsababishia uvimbe kwenye ubongo

HomeElimu

Kufanya ngono kwa mdomo kwamsababishia uvimbe kwenye ubongo

Mwanamke nchini Marekani anayejulikana kwa jina la Amanda amesimulia namna ambavyo mume wake alipatwa na tatizo la uvimbe kwenye ubongo wakati wakiwa wanashiriki tendo la kujamiiana.

Amanda anaeleza kuwa wakati wa mapumziko alitoka na mumewe, Dada yake na shemeji yake na walipofika walichukua chumba kimoja lakini baadae Dada yake na shemeji yake walitoka na kumuacha Amanda na mumewe chumbani.

Amanda anasema “ulikua ni wakati mzuri ambao nilitaka kuutumia na mume wangu, tulianza kufanya mapenzi lakini taratibu mume wangu alianza kupata maumivu, kizunguzungu na kuhisi kama anachanganyikiwa, nilipiga namba ya dharura na mume wangu alifanikiwa kupelekwa hospitali.”

                > Video ya utupu ya Tiwa Savage yavuja, mwenyewe afunguka

Baada ya vipimo mwanaume huyo aligundulika amepata tatizo la “Brain aneurysm’’ ambao ni uvimbe au puto kwenye mshipa wa damu kwenye ubongo, tatizo lililompata kutokana na kufanya mapenzi. Tatizo lililochochewa zaidi na shinikizo la damu alilokuwa nalo miaka 4 nyuma bila yeye mwenyewe kufahamu.

Madaktari walimweleza Amanda kwamba kufanya ngono kwa njia ya mdomo kulisababisha shinikizo la damu kupanda na kusababisha ‘aneurysm’ ambapo matibabu yake yalikua ni  upasuaji.

Upasuaji ulifanikiwa lakini mumewe hakutakiwa tena kushiriki tendo la ndoa.

Ni muhimu kabla ya kuanzisha mahusiano au kukutana kimwili ni vizuri kupima afya kwa kuzingatia vipimo vingi na sio magonjwa ya zinaa peke yake.

error: Content is protected !!