Faida 5 za kujamiiana kwa mjamzito

HomeElimu

Faida 5 za kujamiiana kwa mjamzito

Baadhi ya Wanawake wajawazito wamekuw wazito sana kufanya tendo la ndoa na kutoa sababu mbalimbali za kujitetea bila kujua kwamba wanakosa faida lukuki kiafya kwa kutoshiriki tendo hilo.

Kufanya tendo la ndo kuna faida kadha wa kadha kwa mwanamkae mjamzito na faida zenyewe ni kama zifuatazo;

  1. Hupunguza kwenda ovyo chooni au kujikojolea
    Mtoto anapozidi kuwa mkubwa anazidi kukandamiza kibofu cha mkojo, hii humfanya Mama apate haja ndogo mara kwa mara na wakati mwingine hata akipiga chafya au kukohoa basi mkojo unaweza kutoka wenyewe. Tendo la ndoa huibana misuli ya nyonga na kuzuia hali hii.
  1. Huzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba
    Kuna aina ya Protini inayopatikana kwenye mbegu za Mwanaume ambazo huongeza kinga ya mwili na kuzuia uwezekano wa kupata kifafa cha mimba ambacho kinasababisha kifo kwa Wanawake wengi sana.
  1. Hutibu tatizo la ukosefu wa usingizi
    Wanawake wengi wajawazito huwa na dalili mbalimbali za maumivu na kuumwa sehemu tofauti za mwili pamoja na msongo wa mawazo. Hii huweza kuwakosesha usingizi kabisa. Tendo la ndoa huweza kuwapa usingizi mzuri.

    >  Madhara 7 ya kujamiana wakati wa hedhi

  1. Hutibu tatizo la kufika kileleni
    Kipindi cha ujauzito chuchu za mwanamke na kinembe chake huvimba na kuongezeka hisia maradufu huku kiwango cha homoni za Oestrogen kikiwa juu sana. Hii humfanya kufika kileleni kirahisi sana kuliko mwanzoni.
  1. Huongeza uwezo wa kujiamini kwa mwanamke
    Mwanamke anapokuwa mjamzito huwa anapata hofu sana na kutojiamini na mwili wake. Hua na wasiwasi kwamba mwili wake unaharibika. Kitendo cha mwanaume wake kuendelea kushiriki naye tendo la ndoa humpa kujiamini kwamba mwili wake bado uko kwenye hali nzuri na anapendwa.

Hakikisha unatumia mitindo ‘style’ za tendo la ndoa ambazo hazimuumizi mtoto na Mama, yaani hakikisha haulilalii tumbo hasa mimba ikiwa kubwa. Kuna staili muhimu kipindi hiki kama kuangalia upande mmoja, Mwanamke kuja juu, au Mwanamke kuinama.

error: Content is protected !!