Madhara 7 ya kujamiana wakati wa hedhi

HomeElimu

Madhara 7 ya kujamiana wakati wa hedhi

Kuna tabia ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakijamiiana wakati Mwanamke yuko kwenye mzunguko wake wa hedhi na kuona ni kama jambo la kawaida. Taarifa za kitabibu zikufikie kuwa jambo hili sio la kawaida na kuna madhara ambayo Mwanamke na Mwanaume wanaweza kuyapata kwa kushiriki katika kitendo hicho. Madhara hayo yanaweza kuwa yafuatayo;

  1. Athari ya Kisaikolojia
    Mara nyingi mwanaume atajihisi kuwa anafanya mapenzi katika hali ya uchafu kutokana na uwepo wa damu na hali ya umaji na utelezi uliopo kwenye maumbile ya mwanamke pamoja na harufu ambayo inatoka kwenye damu ya hedhi. Mara nyingi pia Mwanamke hupata hisia za kwamba Mwanaume wake hampendi wala kumjali ila anamtumia kwani Mwanaume anaweza kusubiri mpaka atakapomaliza hedhi ndipo wafanye kitendo hicho.
  2. Maambukizi katika tezi dume (Prostetits)
    Hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa Mwanaume na kwa Mwanamke inaweza kuathiri viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi na mirija ya uzazi kwa ujumla wake. Pia Mwanamke anaweza kuwa na tatizo la PID (PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

    > Faida 3 Mwanaume unapaswa kujua kuhusu mzunguko wa hedhi

  3. Maambukizi ya magonjwa za zinaa
    Kujamiiana katika wakati huu kunaweka hatari kubwa na uwezekano mkubwa wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU, Virusi vya homa ya ini na magonjwa yanayoenea kwa kujamiiana na kugusana na damu.
  4. Uwezekano wa kupata utasa na ugumba kwa wote wawili.
  5. Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake kwa Mwanamke.
  6. Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.
  7. Kuziba kwa njia ya mkojo kwa wanaume.
error: Content is protected !!