Fahamu njia ya uzazi wa mpango kwa kugandisha mayai

HomeElimu

Fahamu njia ya uzazi wa mpango kwa kugandisha mayai

Moja kati ya hofu ya wanawake wengi ni kuchelewa kupata mtoto kwa kuhofia mtoto kukosa virutubisho vya muhimu kwenye ukuaji lakini pia mayai kuzeeka ilihali hawapo tayari kupata mtoto ama kushindwa kupata mtoto pale watakapokuwa tayari.

Wanasayansi walivumbua njia nzuri ya kutatua matatizo hayo kwa kuchukua mayai yaliyokomaa kutoka kwenye ovari na kuyagandisha hadi mama atakapokuwa tayari kutumia.

Unashauriwa kugandisha mayai yako ndani ya miaka 25 hadi 30 na miaka 35 kwa kuchelewa.

Mayai ya mwanamke huzeeka na kupoteza nguvu kadiri ya umri unavyoongezeka na hivyo kugandisha mayai yako ukiwa na miaka 25 inamaanisha kuwa hata ukifikisha miaka 40 mayai yako bado yatakuwa na miaka 25 na nguvu ya kupata mtoto mwenye afya njema.

Mayai mengi huhitajika kutolewa kwa wakati mmoja, wakati mwili wa mwanmke huachia yai moja kwa mwezi.

Wataalamu hulazimika kumpatia sindano kadhaa za dawa mwanamke anayejiandaa kugandisha mayai ili mwili uweze kuandaa mayai mengi kwa wakati nnoja.

Mayai yanapokomaa daktari humchoma sindano mama kwenye mirija ya ovari na kutoa mayai hayo yaliyokomaa kisha huwekwa katika kimiminika cha kuwezesha kutunza kwa muda mrefu kabla ya mayai hayo kuhifadhiwa.

Mwanamke anapokuwa tayari daktari hutumia njia ya ‘In vitro fertilization’ (IV)F ambayo hufanywa maabara yaani mayai yaliyogandishwa huunganishwa na manii ya mwenza wa mwanamke mwenye mayai hayo ama mwanaume aliyechaguliwa na kisha kiinitete kushikizwa kwenye ukuta wa kizazi wa mwanamke naye huendelea kukuza mimba yake kama kawaida.

Hakuna muda maalumu wa mayai kugandishwa. Unaweza kutumia mayai yako uliyogandisha ndani ya miaka 15 hata zaidi.

Huduma hii hutolewa kwa kuanzia $10,000 sawa na shilingi milioni 23.2 za Kitanzania.

error: Content is protected !!