Dalili 7 za kumtambua mtu mwenye msongo wa mawazo

HomeElimu

Dalili 7 za kumtambua mtu mwenye msongo wa mawazo

Si kweli mwenye nuru ya tabasamu usoni ni mwenye furaha moyoni. Watu wengi wanatatizo la msongo wa mawazo lakini mbele ya macho ya watu ni wenye furaha. Msongo wa mawazo unaweza kuchukua hata miaka saba bila kugundulika, hii ni hatari zaidi kwa afya ya mtu.
Ni kwa namna gani sasa tunaweza kugundua dalili za awali za msongo mawazo?

7. Mabadiliko makubwa kwenye kulala
Watu wenye msongo huonesha tabia tofauti kwenye kulala, anaweza kulala muda mrefu kuliko kawaida, au anaweza kuchelewa sana kulala. Muda mwingine hulala katika majira ambayo sio kawaida mtu kulala au kukesha usiku kucha kwa kukosa usingizi.

6. Kupungua au kuongezeka kwa uzito wa mwili
Endapo utaona mabadiliko ya ghalfa hasa katika mwonekano wa mwili wa mtu, inawezekana ikawa moja ya dalili ya msongo wa mawazo. Mtu mwenye msongo anaweza kukosa hamu ya kula chakula na anaweza pia kuongeza zaidi uwezo wa kula chakula kupita kawaida.

5. Mabadiliko ya hulka/tabia
Kama mtu ni mzungumzaji sana, mcheshi au anayependa kufanya mitoko ya matembezi, ni rahisi kutambua kuwa pengine ana msongo wa mawazo kutokana na kubadili ratiba ya maisha yaliyozoeleka kwake. Mtu huyu pia ukiona mawazo yake yameanza kuwa hasi juu ya mambo fulani, ujue kuna uwezekano akawa na msongo wa mawazo.

4. Hasira za haraka
Mtu mwenye dalili za msongo anaweza kuwa na hasira za haraka. Pengine tabia yake ya siku zote ni mtu mwenye bashasha, lakini muda mchache tu anaanza kuwa mtu mwenye hasira na kisirani hata kama mambo ambayo hukuyategemea. Hii ni moja ya dalili ya msongo wa mawazo, ni muhimu kukaa na mtu huyu karibu kwenye nyakati kama hizi.

3. Kuwa na mawazo hasi juu yake
Watu wenye msongo hupitia maumivu makali muda mwingine. Maumivu huwafanya kupoteza tumaini na kuanza kuzungumza mambo hasi juu yao. Muda mwingine anaweza kuzungumza katika hali ya utani, lakini ujumbe unakuwa ni wa kweli kuficha hisia zake nyuma ya utani aliozungumza.

2. Kuchoka sana
Ni kawaida sana kukuta mtu mwenye msongo amechoka au kulalamika kuchoka mara kwa mara. Kwa mtu ambaye msongo wake bado haujakomaa, kuchoka huku kunaweza kukukuchanganya kidogo, kwani anaweza kulala usiku kucha, na bado akawa na uchovu wa hali ya juu aamkapo asubuhi. Ana muda mwingi wa kulala lakini huhisi amelala saa moja tu pindi aamkapo.

1. Anakuwa na wakati mgumu kueleza hisia zake
Wengi hudhani mtu mwenye msongo ni lazima awe na hasira, kuna wengi hawaoneshi dalili ya hasira, bali yeye binafsi anaweza kuwa na hisia ya kuhisi yeye hana maana wala thamani yoyote duniani. Mtu huyu sasa anapokutana na mtu anapotaka kujieleza, hushindwa kabisa kwa kuwa haoni wala hajui chakusema kwa kuwa ameshajitoa thamani kabisa. Ukiona mtu anapata tabu kujieleza na hata akijieleza machozi hayamwishi machoni, basi zingatia sana maisha yake, kuwa nae karibu anaweza kuwa msongo.

error: Content is protected !!