Magonjwa 7 yaliyoua zaidi duniani

HomeElimu

Magonjwa 7 yaliyoua zaidi duniani

Asian Flu (1956-1958)
Vifo milioni 2

Haya ni mafua yaliyoanzia Guizhou, China na yalidumu kwa miaka miwili. Haya mafua yalienea hadi Singapore, Marekani na Hong Kong. Shirika la Afya duniani lilirekodi vifo takribani milioni mbili huku Marekani pekee ikiwa na vifo 69,800.

Pigo la Antonine (165 – 180 AD)
Vifo milioni 5

Chanzo cha maambukizi ya ugonjwa huu haikujulikana ingawa ilisadikiwa pengine ni ndui ama surua. Ugonjwa huu ulienezwa na wanajeshi wa Kirumi waliokuwa wakirejea kutoka Mesopotamia miaka ya 165 hadi 180 baada ya Kristu. Ni pigo ambalo liliua wanajeshi wengi wa Ufalme wa Warumi.

Uviko-19 (2019 hadi sasa)
Vifo milioni 6

Hadi hii leo dunia inaendelea kupambana na kudhibiti ugonjwa huu ulioanza kama mafua, kifua na homa kuendelea kuenea kwa Ugonjwa wa Virusi vya Korona (Covid-19) ugonjwa ulioanzia China na kuenea dunia nzima. Bila kuwepo kwa chanjo ya kuvikabili virusi hivyo, nchi nyingi zilipoteza mamia kwa maelfu ya wananchi wao. Ingawa ugonjwa huu ulianzia China, Marekani ndiyo iliyorekodi vifo vingi zaidi duniani ikiwa na takribani vifo laki tisa, themanini na mbili.

Pigo la Justinian (541-542)
Vifo milioni 25

Janga hili lililotokana na tauni lilikaa kwa kipindi cha mwaka mmoja na linasadikiwa kuua takribani nusu ya wananchii wa Ulaya ambayo ulianza katika Himaya ya Byzantine (Byzantine Empire) na miji kando ya Bahari ya Meditereniani. hii ndio tauni ya kanza kurekodiwa huku ikisababisha vifo vya takribani watu milioni 25.

Ukimwi (2004 – 2012)
Vifo milioni 36

Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) ni janga ambalo linaendelea kukatiza uhai wa watu ingawa kwa sasa baada ya kupatikana kwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo, watu wanaweza kuishi muda mrefu na maambukizi hayo.

kati ya 2004 hadi 2012 maambukizi ya Ukimwi yalienea kwa kasi na elimu ya namna ya kujikinga na kuishi na virusi hivyo ikawa ikitolewa kila kona ya dunia. Hadi kufikia 2020 takribani watu milioni 37.7 walikua wakiishi na Virusi vya Ukimwi huku zaidi ya nusu (58%)wakiwa ni wanawake na mabinti.

Mlipuko wa mafua (1918)
Vifo kati ya milioni 20 -50

Karibu theluthi ya dunia iliathirika na ugonjwa huu uliodumu kuanzia 1918 hadi 1920. Ingawa kwa mwaka 1918 kulikuwa na maambukizi milioni 500 na vifo takribani milioni 25 ndani ya wiki 25 za kwanza. Tofauti na mafua ya aina nyingine haya yalishambulia zaidi watu wenye nguvu na vijana na kuwaacha watoto, wazee na waliodhoofika.

The Black Death ama Kifo Cheusi (1346-1353)
Vifo milioni 75 – 200

Hili ni jina lililopewa tauni iliyopiga Bara la Afrika, Asia na Ulaya. Ingawa kama ilivyoonekana kwa mapigo mengi tauni hii pia ilianzia Bara la Asia. ugonjwa huu unaosababishwa na viroboto wanaotoka kwa panya, waliweza kuzaliana zaidi katika fukwe za bahari ambapo ndipo palipokuwa sehemu za makutano ya watu na kupelekea kusambaa kutoka bara moja hadi lingine na ugonjwa huo kuendelea kusambaa.

error: Content is protected !!