Ya Harmonize yamkuta Miriam Odemba

HomeBurudani

Ya Harmonize yamkuta Miriam Odemba

Mwanamitindo kutoka nchini Tanzania ambaye kwa sasa anaishi Ufaransa, Miriam Odemba anazidi kuonyesha mapenzi yake kwa msanii kutoka lebo ya Konde Gang, Ibraah kwa kuandikia maneno yanayoonyesha kuvutiwa na kijana huyo anayefanya vizuri kwenye muziki.

Miriam ameweka wimbo mpya Ibraah unaofahamika kama Rara na kuaomba mashabiki wamuunge mkono kuuangalia wimbo huo, na mwisho akaandika waraka wa hisia zake za mapenzi kwa ibraah akisema mwili wake upo Ufaransa lakini moyo upo Tanzania kwa kinda huyo wa Konde Gang.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Miriam Odemba (@miriamodemba)

Jambo hili limewaacha wengi na maswali kwani sio mara ya kwanza Miriam Odemba kufanya hivi, ikumbukwe wiki moja iliyopita alim-post Ibraah kwa maneno ya mahaba na kuonyesha jinsi gani anampenda.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Miriam Odemba (@miriamodemba)

Mpaka sasa Ibraah hajamjibu Miriam Odemba mpaka kufanya watu kuhusisha tukio hili kama ambavyo Harmonize anavyofanya kwa Kajala.

 

error: Content is protected !!