Uchumi wa Tanzania kuupita wa Kenya ifikapo 2028

HomeKitaifa

Uchumi wa Tanzania kuupita wa Kenya ifikapo 2028

Kinyanga’nyiro cha ukuu wa kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki kinatarajiwa kuchukua mkondo wa ushindani zaidi huku makadirio yakionyesha Tanzania kuipiku Kenya katika miaka 10 ijayo.

Ripoti liyotolewa hivi karibuni na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania ambao sasa unafikia dola za kimarekani bilioni 85.4 unatarajiwa kukua hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 136 ifikapo mwaka 2028.

Katika viwango vya sasa, uchumi wa Tanzania ni mkubwa kuliko baadhi ya nchi ndogo za Ulaya kwani mwaka 2023 uchumi umekua hadi $85.42bn kutoka $69.94bn mwaka 2021, ripoti ilibainisha.

error: Content is protected !!