Madadapoa wamaliza mavuno Shinyanga

HomeKitaifa

Madadapoa wamaliza mavuno Shinyanga

Wanawake katika vijiji wilayani Shinyanga, wa,elalamika kitendo cha madadapoa maarufu ‘machangudoa’ kutoka mjini kwenda huko kipindi cha mavuno, kufanya biashara ya kujiuza kwa kubadilishana na mazao kama mpunga.

Wanawake hao kutoka vijiji vya Lyamidati na Lyabukande wilayani Shinyanga, walipaza sauti hizo juzi kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo wa namna ya kupambana na matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yaliyotolewa na Shirika la Agape.

Mmoja wa wanawake hao , Matha Malale alisema kipindi cha masika familia zao zinakuwa na upendo, lakini msimu wa mavuno ukifika migogoro inaanza kuibuka.

“Matukio mengi ya ukatili wa kijinsia ambayo yapo huku vijijini ni wanaume kutelekeza familia huku chanzo chake kikubwa kikitajwa kuwa ni wimbi la madadapoa kutoka mjini ambao wanaokwenda vijijini kipindi cha mavuno kwa ajili ya kufanyabishara ya ngono kwa kubadilishana na mazao,” alisema Matha.

Madadapoa hao wanawapa masharti kwamba wakitaka kuona maumbile yao, wanatoa debe moja la mpunga na wakifanya tendo moja la ngono wanalazimika kulipa gunia moja la mpunga na kwamba katika msimu mmoja anazokusanya kutoka kwa wanaume inakadiliwa kuwa wanakusanya zaidi ya gunia 100 huku familia zikibaki na njaa.

Meneja miradi kutoka Shirika la Agape, Peter Amani aliwataka wanaume wa maeneo hayo ya vijini kuachana na mila kandamizi ambazo zimekuwa chanzo cha migogoro na ukatili ndani ya familia kwa kumnyima sauti mwanamke pamoja na kuwa na haki ya kusimamia mavuno ya mazao.

Baadhi ya wanaume wamekiri kutumia mazao pamoja na mifugo katika masuala ya ngono na kwamba kinachowasumbua ni ulimbukeni wa kupenda wanawake wa mjini sababu ya udhanifu wao na kuwapa mapenzi mazuri.

error: Content is protected !!