Apata ajali, mkono washonewa tumboni

HomeKimataifa

Apata ajali, mkono washonewa tumboni

Maisha ni kama fumbo tunaamka wazima hatujui tutakutana na nini na wakati gani.  Ni sawa na Martin Shawn wa  nchini Uingereza ambaye alipata ajali mbaya ya gari, September 9 mwaka huu.

Gari lake lilipinduka mara nne na kumsababaishia majeraha makubwa kwenye mkono wake ambao ilibidi afanyiwe upasuaji, mkono wake uliunganishwa na tumbo lake ili kumsaidia kupona haraka.

Baada ya ajali Shawn alipelekwa hospitali katika mji wa Leicester anasema, “Nilikua sijui nini wanataka kufanya kwenye mkono wangu ila nilikua tayari kwa lolote kwaajili ya kunusuru mkono wangu. Madaktari walitumia kipande cha nyama ya tumbo langu na kukishonea kwenye mkono pamoja na tumbo ili kusaidia tishu za mkono kukua haraka, kitaalamu inajuliakana kama “Fediclep flap”.
Daktari aliyemfanyia Shwan upasuaji, Mr Patel anasema njia hiyo hawaitumii sana katika mazingira ya sasa. Njia hiyo ilikua inatumika zamani zaidi haswa kwenye vita Shawn alifanyiwa operasheni hiyo ili kumsaidia kuweza kutumia tena mkono wake kwani sehemu kubwa ya mkono kwenye maeneo ya kiganja ilikua imeharibika.

error: Content is protected !!