Fetty Wap akamatwa na dawa za kulevya

HomeBurudani

Fetty Wap akamatwa na dawa za kulevya

Rapa Willie Junior Maxwell II maarufu kama Fetty Wap (30), amekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na genge la uuzaji wa dawa za kulevya mjini New York.

Hati za upelelezi uliofanyika wakati wa uchunguzi zilipata takriban Bilioni 2 na nusu, kilo 16 za kokeini, kilo mbili za heroini, tembe nyingi za ‘fentanyl’, bastola mbili, bunduki, na risasi kadhaa.

Fetty Wap alikana hatia lakini amekosa dhamana na kubaki kizuizini.

Kwa mujibu wa sheria za nchini Marekani, iwapo Fetty Wap na washtakiwa wote watakutwa na hatia, watakabiliwa na hukumu ya hadi kifungo cha maisha jela.
Fetty Wap aliwahi kutamba na wimbo wake wa “Trap Queen” uliofanya vizuri na kushika nafasi ya 2 kwenye chati za Billboard mwezi Mei 2015.

error: Content is protected !!