Nyota wa Ponografi amuomba Elon Musk

HomeBurudani

Nyota wa Ponografi amuomba Elon Musk

Nyota wa zamani wa ponografi amesema, Elon Musk anahitaji kupiga marufuku maudhui ya picha na video za utupu kwenye mtandao wa Twitter.

Lisa Ann, 49, amemhimiza tajiri mkubwa zaidi duniani kushughulikia tatizo hilo wakati unyakuzi wake wa pauni bilioni 43 wa mtandao wa kijamii utakapoidhinishwa.

Mtumbuizaji huyo wa zamani wa picha na video za utupu amesema ni rahisi sana kwa watoto na vijana kupata maudhui machafu wanapotumia Twitter.

Akizungumza kwenye podikasti yake, Lisa – jina halisi Lisa Ann Corpora – alisema hapingani na ponografia. Lakini anapinga kupatikana kwa watazamaji wa umri wa chini.

Kwa sasa, Twitter hairuhusu mtu yeyote aliye chini ya umri wa miaka 13 kuunda akaunti katika jitihada za kuzingatia GDPR, lakini mtumiaji kuongeza siku yao ya kuzaliwa, hivyo inawezekana kudanganya mfumo.

Walakini, Musk anasema anataka kuifanya kampuni hiyo kuwa ya kibinafsi ili kuondoa akaunti bandia.

Kwa hivyo kunaweza kuwa na matumaini bado kwamba Twitter inaweza kusafisha shida yake ya ponografi.

 

error: Content is protected !!