Kikao cha dharura kushusha bei ya mafuta

HomeKitaifa

Kikao cha dharura kushusha bei ya mafuta

Kufuatia malalamiko ya wananchi kutokana na kupanda kwa kasi kwa  bei za mafuta kulikopelekea pia kupanda kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali nchini, usiku wa Mei 8, Rais Samaia Suluhu Hassan akaitisha kikao cha dharura Ikulu, Dar es Salaam.

Amewaagiza  viongozi waliohudhuria kikao hicho kutafuta utatuzi wa tatizo hilo la mfumuko wa bei ya mafuta nchini.

Viongozi waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata, na makatibu wakuu wao.

error: Content is protected !!