GAIRO: Madarasa 12 ya Samia yavunjwa vioo

HomeKitaifa

GAIRO: Madarasa 12 ya Samia yavunjwa vioo

Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabir Makame amemsimamisha kazi Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibedya, wilayani humu, Kelvin Kayombo ili kupisha uchunguzi baada ya madarasa 12 yaliyojengwa kwa fedha za Mpangao wa Maendelo wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19, maarufu kama madarasa ya Mama Samia, kuhujumiwa kwa kuvunjwa vioo.

“Tulimhoji mlinzi wa shule na mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, alikiri siku ya tukio hakuwapo eneo lake la kazi, lakini mbaya zaidi shule imefungwa miundombinu ya umeme, siku ya tukio hakukuwa na umeme, kumbe luku imeisha muda mrefu ma uongozi wa shule haukuhangaika kununua,” alisema Makame.

Licha ya kukamatwa kwa watu haona kusimamishwa kazi kwa mkuu wa shule, Mkuu wa wilaya pia ameagiza watu wote waliohusika na uharibifu huo kulipa gharama za kuweka upya vioo vilivyovunjika wakati mashauri yao yakiendelea kwenye vyombo vya dola.

Taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa kuvunjwa vioo hivyo kumetokana na wivu wa kimapenzi baada ya mtuhumiwa kumtuhumu mlizni wa shule kuwa na mahusiano na mkewe, hoja ambayo licha ya kutanjwa na viongozi na wanakijiji, imeshindwa kuthibitishwa na kamanda wa Polici Mkoa wa Morogoro, SACP Fortunatus Musilim.

error: Content is protected !!