Madaktari wapendekeza chanjo ya UVIKO-19 iwe lazima

HomeKitaifa

Madaktari wapendekeza chanjo ya UVIKO-19 iwe lazima

Katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19, waganga wakuu wa mikoa wameishauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, iangalie uwezekano wa kuifanya chanjo ya ugonjwa huo kuwa ya lazima.

Wito huo wameutoa kufuatia vifo vinavyoendelea kuwakumba baadhi ya wataalamu wa afya walio mstari wa mbele katika kutoa huduma kwa wagonjwa, tangu ugonjwa huo uingie nchini Machi 2020.

Akisoma risala katika ufunguzi wa kikao chao kilichofanyika jijini Dodoma, Katibu wa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri, Dkt. Japhet Simeo alisema tangu kuanza kwa janga hilo, nchi imepoteza wataalamu muhimu wa afya waliokuwa mstari wa mbele kuwahudumia wagonjwa wa Uviko-19.

“Kutokana na umuhimu wa chanjo katika kukabiliana na UUVIKO-19 tunashauri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, iangalie uwezekano wa kuifanya chanjo hii kuwa ya lazima kwa watu wote wenye vigezo vya kuchanjwa” alisema.

error: Content is protected !!