Je? ‘Love Bite’ inaweza kukuua?

HomeElimu

Je? ‘Love Bite’ inaweza kukuua?

Julio Macias Gonzalez, umri miaka 17, alifariki Dunia kwa kiharusi (Stroke) baada ya kupigwa busu la shingo kwa mtindo wa kunyonywa (Love Bite) na mpenzi wake na umri wa miaka 24. Tukio hili lilitokea mnamo mwaka 2016 huko nchini Mexico. Kituo kimoja cha habari nchini humo kiliripoti baada ya tukio hilo kuwa, kifo hicho kilisababishwa na damu kuganda eneo la shingo, eneo lililonyonywa hivyo kuzuia damu kupita kuelekea kwenye ubongo na kupelekea kufariki.

Kufuatia tukio hilo, watu wengi duniani wamejenga hofu juu ya tendo hilo, na wengine wamekuwa wakisambaza uvumi kuwa unaweza kupoteza maisha kama utafafanya kitendo hicho kiasi cha kusababisha kutoa alama nyekundu shingoni au eneo lingine la mwili.

Charles Adams, Rais mtaalamu wa masuala ya damu ya binadamu (Hemetologist) amesema kuwa kuna uwezekana mdogo sana busu la kunyonya kusababisha kifo, ila inawezekana tu endapo tayari mtu anayenyonywa atakuwa na hitilafu kwenye mishipa yake ya damu. Hitilafu hiyo inaweza kupelekea mishipa kupasuka pindi anapokuwa ananyonywa na mwenza wake. Dkt. Charles amesema lakini hafikiri kama inaweza kutokea watu kama watu wote watakuwa wazima kabisa kiafya.

Daktari anaendelea kusema kuwa uwezekano wa kufa kwa busu tu uko chini ya asilimia 1, lakini sio kwamba haiwezekani, lakini hadi mtu akifa kutokana na hilo, uje tayari kuna mrundikano wa matatizo mengi tayari kwa mtu huyo.  Kuganda kwa damu hutokea kwenye mishipa ya damu yenye kazi ya kupeleka damu kwenye moyo, na ile inayoitoa damu kwenye moyo kwenda kwenye ubongo. Pindi mishipa hiyo inapopungua upana kutokana na kuganda mafuta kwenye kuta zake, hivyo kupunja kiwango kinachotakiwa kwenye moyo ubongo au moyo na kupelekea shinikizo la damu au kiharusi.

Daktari anasema hadi kufikia hatua hii sio suala la siku moja, bali ni mfululizo wa matukio na mtindo wa maisha, hivyo kwa busu kuwa chanzo kikuu cha kiharusi ni suala gumu na adimu sana kutokea. Ingawa, daktari hakukataa kabisa kama busu haliwezi kusababisha mauti, alisema inawezekana endapo mtu atanyonywa kwa muda mrefu na kwa kutumia nguvu kwenye maeneo ya shingo ambayo hupitisha damu kuelekea kwenye ubongo. Kama mishipa hiyo inaminywa na kushindwa kusafirisha damu kwa ufanisi kwa muda mrefu, mtu anaweza kupoteza maisha.

Hata hivyo, amewataka watu wasiogope, kwani sio tukio linalotokea sana, na hatari yake ni ndogo sana, hivyo ni muhimu kupima afya zetu mara kwa mara na kufanya mazoezi mepesi kuweza kujilinda na hatari kama hizo ambazo zinaweza kujitokeza.

error: Content is protected !!