Bilionea namba moja Afrika Mashariki

HomeKimataifa

Bilionea namba moja Afrika Mashariki

Tanzania imeipiku Kenya kwa kutoa mfanyabiashara bilionea katika sekta binafsi ikiwa ni kwa mujibu  wa ripoti ya mwaka 2022 iliyotolewa na Kampuni inayohusika na mambo ya uwekezaji ya Henly and Partners, Tanzania katika viwango vya uwekezaji wa sekta binafsi imekuwa ya sababu huku Kenya ikiwa ya tano. 

Kwa sasa rekodi hiyo inashikiliwa na mfanyabiashara maarufu Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye tayari pia jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea namba moja Afrika Mashariki na akiwa miongoni mwa mabilionea Afrika kufuatia utajiri wake kufikia dola bilioni 1.6.

Mo ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mohamed Enterprises (MeTL), iliyoanzishwa miaka ya 1970, kwa sasa ina matawi katika nchi sita za Afrika huku ikihusika pia na biashara mbalimbali. 

error: Content is protected !!