Hiki ni kijiji mkoani Tanga ambacho makaburi yamefukuliwa na maiti kuibwa

HomeKitaifa

Hiki ni kijiji mkoani Tanga ambacho makaburi yamefukuliwa na maiti kuibwa

Wananchi wa Mtaa wa Bwila, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga wameiomba serikali kuingilia kati na kutafuta ufumbuzi wa tatizo lao kwani watu wasiojulikana wamekuwa wakifukua makaburi ya ndugu zao na miili ya ndugu zao kutoonekana.

Taarifa hizo zimeibuliwa baaada ya kufukuliwa kwa makaburi mawili na miili kutokuonekana.

Rehema Lugundi ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema makaburi yaliyofukuliwa ni ya wajukuu zake ambao ni mapacha, walizikwa mwezi mmoja kabla ya tukio hilo kufanyika.

Kutokana na kufukuliwa kwa makaburi hayo, Omari Hamza yeye amethibitisha kuona mwili wa mtoto mdogo mtaani kwao baada ya kupokea taarifa kutoka watoto anaowafundisha madrasa. Amesema aliopeenda kuangalia hakukuta mwili ila inasadikika kwamba huenda mwili huo ukawa umechukuliwa na mbwa kwani sanda ilikuwa imebaki katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bwila, Shabani Mgaza amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. “Ni kweli baada ya kupata taarifa hizi nilifika na wananchi eneo la tukio, tulikuta makaburi mawili yamefukuliwa na  tulipokagua tulikuta sanda tu, ila mabaki ya miili ya watoto waliozikwa haipo imetolewa na wahusika walirudishia tu udongo.”

error: Content is protected !!