Achoma nyumba moto kisa mapenzi

HomeKitaifa

Achoma nyumba moto kisa mapenzi

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Kida, mkazi wa jijini Tanga, anadaiwa kuchoma moto nyumba ya mama mzazi wa mpenzi wake.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Septemba 21, 2021 katika eneo la Chumbageni jijini Tanga, chanzo kikielezwa kuwa ugomvi wa kimapenzi kati ya Kida na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Stella.

Wakielezea kuhusu tukio hilo, wapangaji katika nyumba ilichomwa moto, wamesema walimuona kijana huyo akiwa na dumu lenye mafuta ya petroli takriban lita 20, ambapo alianza kutukana na kutoa vitisho, kisha akamwaga petroli hiyo na kuchoma moto nyumba hiyo.

Majirani na mashuhuda wa tukio hilo wameiomba Serikali kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba mhusika analipa fidia kutokana na hasara aliyosababisha, hasa ukizingatia kwamba mama mwenye nyumba hiyo ni mjane anayetegemea nyumba hiyo kama chanzo chake cha kipato.

error: Content is protected !!