Mbinu 3 rahisi za kutongoza mwanamke na kukubali bila vikwazo

HomeElimu

Mbinu 3 rahisi za kutongoza mwanamke na kukubali bila vikwazo

Moja ya changamoto wanayokutana nayo wanaume wengi ni kwa namna gani wanaweza kutongoza mwanamke na hatimaye akakubali. Wengi wao wanakosa ujasiri na nguvu ya kujiamini kutongoza mwanamke ana kwa ana, na kuishia kuomba namba ya simu.

Sasa ili kuwaponya domo zege walio wengi hii ndiyo tiba ya kutongoza mrembo yeyote hatimaye akakukubali.

1. Kuwa karibu naye
Siku zote , kama unataka kumtokea mwanamke njia muhimu kabisa ni kuweza kumjua kwa undani .Usikurupuke kurupuke tu ukaanza kutongoza , mwanamke bila kujua tabia yake, vitu anavyopendelea kwa maana ataogopa au atakuona mtu rahisi kuwa naye na mwisho wa siku utaishia kuumbuka.

2. Usionyeshe udhaifu
Wanaume wengi huwa wanafanyaga kosa hili kubwa, wanawaambia wanawake wanawapenda au wanahisia za kimapenzi kwao. Ni kweli unampenda , anajua hivyo tayari. Epuka kuwa na papara kwa maana unaonyesha kutokukomaa kwako.
Japokuwa anahisi unampenda, usijaribu kuonekana hivyo kwani anahitaji kusikia kutoka kwako ili ajihikikishie hisia zake. Chukulia poa na usifunguke kuhusu hisia zako kwake , kitendawili alichonacho ndicho kitamfanya azidi kukunata na kutaka kujua mwisho wa mambo.

> Fahamu mbinu inayotumika kumtambua rafiki wa kweli kwenye mafanikio

3. Jiamini  na uache uongo
Unapoongea nae usiku , mwaga sera zako na funguka kuhusu mambo ya mapenzi ila mnapokutana ana kwa ana mchana usiongelee mambo ya mapenzi kabisa labda aanze yeye na hivyo kumaanisha ashaingia line na anapenda maongezi hayo.

Epuka kuongelea kuhusu mambo yenu ya kimapenzi mnapokua na marafiki wengine bali fanyeni hivyo mkiwa wawili. Kwa kufanya hivyo unamfanya aamini kuna uhusiano motomoto kati yenu.

Ongea nae na upate kumjua vizuri . Mtumie message na usiwe na mzuka , mfanye awe kama rafiki kwanza . Usimtokee kwanza sema pia usisubiri sana maana ataanza kukuchukulia poa .

error: Content is protected !!