Mohamed Ibrahim: Kijana wa miaka 36 aliyezama kwenye penzi la Kikongwe wa miaka 82

HomeKimataifa

Mohamed Ibrahim: Kijana wa miaka 36 aliyezama kwenye penzi la Kikongwe wa miaka 82

Iris, kikongwe wa miaka 82, anaonekana mwenye furaha kila amzungumziapo mume wake wa ndoa, Mohamed Ibrahim raia wa Misri mwenye miaka 36.

Mohamed alifunga ndoa na Bi. Iris jijini Cairo mnamo 2020, Iris raia wa Uingereza alipendana na Mohammed kupita mtandao wa kijamii wa Facebook, hadi kikongwe huyo kuamua kufunga safari hadi Misri kukutana na kijana huyo hatimaye wawili hao kufunga ndoa.

Kila uchwao, kilio cha Bibi Iris ni juu ya mamlaka ya uhamiaji nchini Uingereza kuchelea kumpa kibali cha makazi (VISA) mumewe aliyetenganishwa nae takribani maili 5,864.

> Penzi la kweli linavyoitikisa ngome ya kifalme Japani

“Nimetenganishwa na mtu ninaye mpenda kwa dhati, sijakata tamaa na uzee wangu bado, ila naweza kufa hata kesho, kila sekunde ina thamani kwangu, naumia sana”. Iris aliliambia Jarida la Metro

Mohamed naye akieleza hisia zake, ameonesha kukolea kwa penzi la Iris huku akitamka wazi kuwa aliacha kazi zake zote na kutumia muda wake mwingi na Iris pindi alipokuwa Cairo, hivyo anamkumbuka kila dakika na anatamani aungane naye wakati wowote.

Katika hali isiyo ya kawaida, kikongwe huyo aliwahi kusema katika kituo kimoja cha runinga nchini Uingereza, kuwa usiku wake wa kwanza kulala na Mohamed, walitumia kichupa chote cha kilichojaa kilainishi, hivyo kila akiwaza siku hiyo, upweke unazidi kumuandama na huenda akafariki mapema zaidi kama atamkosa mume wake.

error: Content is protected !!