Sababu zinazoweza kufanya msichana akubali kuwa nyumba ndogo

HomeMakala

Sababu zinazoweza kufanya msichana akubali kuwa nyumba ndogo

Kuwa nyumba ndogo (side chick) ni kitendo cha msichana au mwanamke kukubali kuwa katika mahusiano na mwanaume ambaye ana mahusiano yaliyo rasmi zaidi

1. Urahisi

Msichana anaweza kukubali kuwa nyumba ndogo kwani atahisi urahisi kwanye masuala mbalimbali ya kimahusiano.

Wepesi unaweza kupatikana hasa katika masuala ya migogoro na mijadala mingine inayohusu matatizo kwani mambo hayo hupelekwa zaidi kwa nyumba kubwa (main chick)

2. Kupewa muda mwingi (Attention)

Jarida la Pulse la nchini Nigeria limefanya utafiti mdogo kwa kuzungumza na wasichana ambao walisema kwamba wanaweza kukubali kuwa nyumba ndogo kwa mwanaume ambaye anajali na kutumia muda wa kutosha kwa ajili ya mahusiano.

Wasichana hao wamedai ni bora kuwa na mtu ambaye ana mahusiano mengine, kuliko kuwa na mwanaume ambaye hajali

3. Sababu za kiuchumi

Baadhi ya wasichana hutafuta zaidi faida za kiuchumi kuliko mapenzi. Iwapo mwanaume atawapa fedha na kukidhi mahitaji mengine, wako tayari kuruhusu awe na wanawake wengine.

4.  Kuridhishwa katika tendo la ndoa

Jarida la Pulse la nchini Nigeria linaeleza kwamba wasichana wengi wamejikuta wakikubali kuwa nyumba ndogo kwa wanaume ambao wanawaridhisha kwa viwango vya juu wanapojamiiana.

5. Kuchelewa kufahamu ukweli

Wapo wasichana ambao waliingia kwenye mahusiano na wanaume wenye ndoa au mahusiano mengine, lakini wameshindwa kutoka kwa sababu ya kuchelewa kufahamu ukweli wa mambo.

Wanapofahamu ukweli huo wanakuwa tayari wamewekeza hisia na mambo na mambo mengine yanayowawia vigumu kuyaacha.

error: Content is protected !!