Ishara kuwa hana mpango na wewe

HomeElimu

Ishara kuwa hana mpango na wewe

Kabla ya kujiingiza kwenye mahusiano kwaajili ya kuanza maisha na mtu, ni muhimu kujua ni mtu wa aina gani unamtaka na kujua wakati gani wa kuachana na hayo mahusiano.

Upo wakati upo kwenye mahusiano na mtu ukiwaza kujenga familia na huyu mtu ilihali yeye hajioni akitengeneza familia muda wowote na zaidi hajioni akianzisha familia na wewe. Wakati wote huu zipo ishara zinazoonesha kuwa si wakwako ila wewe tu ndio unashindwa kukubaliana na ukweli.

Anaonesha upendo kwako lakini haongelei mpango wa kwenda kwenye hatua inayofuata. Mtakuwa kwenye mahusiano hata miaka mitatu lakini hana uhakika wa nini kinafuata, hajui lini ataoa, Je! Ni wewe atakuoa lakini anafurahi kuwa na wewe kwenye maisha yake.

Kamwe haulizi kuhusu maisha yenu ya baadaye. Wewe ndio unayewaza na kuuliza mahusiano haya yanaenda wapi? nini malengo ya ninyi kuwa kwenye mahusiano na je wote wawili mna mipango ambayo ikiwekwa mezani mnaweza kutimiza mipango  mingi kwenye umoja wenu? Yeye anahesabu tu yupo kwenye mahusiano na wewe kama vile mtu aliyepanda daladala na hajui wapi linaelekea.

Hakutambulishi kwa watu wake wa karibu. Mpo kwenye mahusiano lakini hawezi kukutambulisha kwa ndugu au marafiki zake wa karibu wala hujui kanisa analosali. Anaweza pia kukutambulisha kwa baadhi ya marafiki zake ambao unaona kuwa hawana tabia za kuridhisha au mjomba ambaye huoni heshima ya mtu na mjomba wake. Yaani anatafuta njia ya kufichaficha vitu vingine kwako.

Kuna mambo inabidi akamilishe kwanza kabla ya kuanza kuwaza kuanzisha familia na wewe. Atakupa kila aina ya sababu, ngoja nimalize nyumba, kuna deni kubwa nikamilishe, nasomesha wadogo zangu, nikishakuwa na pesa kiasi fulani na gari, yani hakaukwi sababu za kuchelewesha hili jambo ama kupeleka siku mbele.

Pengine mnaendana kwa kila kitu lakini ni wakati tu ndio tatizo. Tunaendana na tunapendana lakini ndani ya mwaka mmoja ungependa kuwa kwenye hatua fulani ya maisha kwenye mahusiano yako lakini mwenzio ana mipango hiyohiyo na wewe baada ya miaka mitatu. Jua tu si wakati wenu na pengine ni muda sasa wa ninyi kufikia muafaka wa kuachana na hayo mahusiano.

Usiruhusi hisia zako kukufanya uchague mtu asiyesahihi kwa malengo yako ya maisha.

error: Content is protected !!