Zamaradi: Mwijaku anaupiga mwingi

HomeBurudani

Zamaradi: Mwijaku anaupiga mwingi

Mkurugenzi na Mmiliki wa Zamaradi TV, Zamaradi Mketema amempa pongezi mtangazaji wa redio ya Clouds, Mwijaku kwa kuwamwambia anafanya kazi nzuri sana hasa katika kuhamasisha Watanzania kuungana na Rais Samia Suluhu kwenye uzinduzi wa filamu inayoonyesha vivutio vya kitalii vya Tanzania iliyopewa jina la Royal Tour itakayoonyeshwa kesho Aprili 28, 2022 jijini Arusha.

Kupitia ukurasa wake wa Tiwtter, Zamaradi alimtaja Mwijaku kama mtu asiyekata tamaa na mwenye bidii kwa kila anachofanya.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Zamaradi Mketema (@zamaradimketema)

Filamu ya Royal Tour ambayo muhusika mkuu ni Rais Samia Suluhu Hassan, ilizinduliwa kwa mara ya kwanza New York, Marekani na sasa ni zamu ya Tanzania ambapo itaonyeshwa kesho jijini Arusha.

error: Content is protected !!