Diamond kufuturisha bungeni

HomeBurudani

Diamond kufuturisha bungeni

Msanii na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, leo Jumatano Aprili 27,2022 anatarajiya kufuturisha waheshimiwa wabunge jijini Dodoma, taarifa iliyotolewa katika mkutano wa saba kikao cha kumi na tatu wakati wakitambulishwa wageni waliohudhuria Bunge hilo.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson alimtambulisha Diamond pamoja na watu alioongozana nao huku akimpongeza kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuitangaza Tanzania kisanaa na pia kuwaajiri watu kwenye kampuni yake ya Wasafi Media.

“Tunakushukuru sana Diamond Platnumz kwa sadaka hii ambayo umekuja kuitoa kwa waheshimiwa wabunge asante sana, lakini pia tunatambua mchango wako mkubwa katika sanaa nchi hii, hasa sanaa ya muziki na ajira ulizozitoa hapo. Nilikua nasoma orodha ya watu ambao umewaajiri wewe umefanya kazi nzuri tunakupongeza sana na tunakutakia kila la heri katika mipango yako uliyo nayo ya huko mbele kuendeleza sana lakini pia kuendelea kuajiri vijana wa nchi hii,” amesema Spika Tulia.

Diamond ameengozana na Mama yake mzazi, Bi. Sandra, Esma, Lil Ommy, Mo Town Sanya, Mkubwa fella, Ricardo Momo, Don Fumbwe, Uncle Shamte, Mkubwa Fella, Dida Shaibu, Juma Lokole na wafanyakazi wengine.

error: Content is protected !!