Mbunge auawa kwa kuchomwa kisu

HomeKimataifa

Mbunge auawa kwa kuchomwa kisu

Mbunge wa Chama cha Wahafidhina (Conservative) nchini Uingereza, Sir. David Amess amefariki baada ya kuchomwa visu mara kadhaa wakati akifanya ziara za vikao jimboni kwake Essex.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 25 anayeshukiwa kutekeleza mauaji hayo katika Kanisa la Leigh-on-Sea. Polisi wamefanikiwa kupata kisu kilichotumika kwenye mauaji hayo.

Mbunge huyo aliyekuwa na umri wa miaka 69, amekuwa Mbunge katika eneo hilo tangu mwaka 1983 na ana mke na watoto watano.

Katibu toka Wizara ya Afya Uingereza, amesema Sir. David alikuwa kiongozi mwadilifu na ameuawa wakati akitekeleza wajibu wa kidemokrasia. Licha ya wauguzi wa huduma za dharura kujaribu kuoa maisha yake, imeelezwa kuwa David alifia eneo la tukio.

error: Content is protected !!