Rais Samia awataka wananchi wa Kilimanjaro kudumisha amani na upendo

HomeKitaifa

Rais Samia awataka wananchi wa Kilimanjaro kudumisha amani na upendo

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa mkoani Kilimanjaro kudumisha amani ili kuipa Serikali nafasi ya kutatua changamoto zao akiwa kwenye  uzinduzi wa barabara ya lami ya Sanya Juu–Elerai, Siha Mkoani Kilimanjaro yenye urefu wa kilometa 32.2.

“Nawaomba dumisheni amani na utulivu kwenye maeneo yenu ili Serikali tupate wasaa mzuri wa kufikiri wapi tupate fedha ili kumaliza changamoto zinazowakabili.” amesema Rais Samia

Pia Rais Samia ameweka  msisitizo kauli yake kwa kusema haipendezi kukuta changamoto za wananchi zinajirudia kila wakati hata baada ya kutatuliwa na Serikali Kuu, na kuongeza kwamba ni vyema serikali ya eneo husika kushirikiana na Mkoa katika kumaliza changamoto hizo.

Mbali na hayo Rais Samia amewataka viongozi kusimamia utatuzi wa changamoto zinazotatuliwa na Serikali Kuu pamoja na Chama kusudi zisijirudie mara kwa mara.

error: Content is protected !!