Sabaya alivyowataja Magufuli na Mpango mahakamani kwenye utetezi wake

HomeKitaifa

Sabaya alivyowataja Magufuli na Mpango mahakamani kwenye utetezi wake

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya leo Ijumaa tarehe 15 Oktoba amehukumiwa miaka 30 Jela kwa makosa ya Unyang’anyi wa kutumia silaha. Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo.

Tarehe 13 Agosti 2021 katika Mahakama ya Hakima Mkazi Arusha Sabaya aliwataja aliyekuwa Rais wa awamu ya 5, Hayati Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na Gavana wa Benki Kuu kuwa walikuwa wanajua operesheni aliyokuwa anaifanya Arusha.

Sabaya amesema hayo wakati akitoa utetezi mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo kuwa alichokuwa anakifanya Arusha Februari 9, 2021 haikuwa operesheni yake ya kwanza kuagizwa na hayati Rais Magufuli.

  > Sabaya jela miaka 30

Akiongozwa na Wakili anayemtetea Mosses Mahuna, wakati alipoanza kujitetea mahakamani hapo amesema kesi hiyo ni ya kutengeneza na yeye hajaiba wala kumtishia mtu yoyote kwa silaha.

Sabaya alisema siku ya tukio Februari 9, 2021 alipomaliza kuongoza kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai, alipokea simu ya Dkt Magufuli aliyemwelekeza kazi ya kufanya katika mkoa wa Arusha ambapo pia alipaswa kuwapitia watu wengine wanne katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo watu hao walikuwa na maelekezo juu ya kazi hiyo wanayoenda kufanya.

“Hiyo haikuwa kazi ya kwanza kwa sababu miezi michache iliyopita tulipewa zoezi la kukamata mitambo inayotengeneza noti bandia na tulifanikiwa kukamata mitambo na fedha Sh 800 Milioni bandia eneo la Chanika wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, Gavana wa BOT anajua na aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa wakati huo Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa sasa pia anafahamu.”

error: Content is protected !!