Youtube ya Diamond Platnumz yafutwa

HomeBurudani

Youtube ya Diamond Platnumz yafutwa

Ikiwa ni siku mbili tangu kudukuliwa kwa akaunti ya Youtube ya msanii Diamond Platnmuz, leo Jumatatu Aprili 25,2022 akaunti hiyo imefutwa katika mtandao huo na wamiliki.

Youtube ya Diamond yadukuliwa

Ingawa ilifanikiwa kurudishwa baada ya kudukuliwa sasa hivi haipo kabisa Youtube.

Muonekano wa akaunti ya Youtube ya Diamond Platnumz

Kwa sasa ukifungua akaunti hiyo unakuta ujumbe kwamba Akaunti haipo kwa sababu imekiuka masharti.

Kabla ya Diamond kudukuliwa akaunti yake hiyo, msanii mwingine kutoka lebo ya Wasafi, Mbosso naye alipatwa na shida hiyo ingawa alifanikiwa kuirudisha.

error: Content is protected !!