Youtube ya Diamond Platnumz yadukuliwa

HomeKitaifa

Youtube ya Diamond Platnumz yadukuliwa

Msanii wa Bongo Fleva kutoka Tanzania Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii wanaofuatiliwa zaidi Afrika Mashariki na mmiliki wa lebo ya Wasafi ambayo imesajili wasanii wengine kadhaa wanaofanya vizuri. 

Asubuhi ya leo ilikuwa siku mbaya sana kwa msanii huyo maarufu baada ya akaunti yake ya YouTube iliyo na watumiaji zaidi ya 6.35M kudukuliwa na kikundi cha Bitcoin na wataalamu wengine wa biashara ya pesa ambao waliipa jina Tesla, kuandaa tukio la moja kwa moja na kuzima sehemu ya maoni.

Tukio kama hili lilitokea kwa chombo maarufu cha habari cha Kenya, Citizen Tv mwezi mmoja uliopita na watu wale wale waliingia katika Akaunti yao ya YouTube na kutayarisha tukio la moja kwa moja.

Timu ya IT ya Diamond Platnuzm  ililazimika kufanya juhudi za haraka sana kurejesha akaunti hiyo na walifanikiwa  hilo baada ya muda wa dakika arobaini na tano. Wadukuzi hao pia walizuia tukio lake la moja kwa moja huku wakilihusisha na madai ya hakimiliki ya DSTV.

Mpaka sasa Uongozi haujazungumza lolote kupitia kitendo hicho hata mtaalamu wao wa Upande huo pia Tunasubiri kauli yoyote kutoka kwao.

 

error: Content is protected !!