Vitabu 10 vya kukuza akili

HomeKitaifa

Vitabu 10 vya kukuza akili

Kama ilivyo kwa mtu kwenda gym au kukimbia ili kuimarisha misuli ya mwili, ndivyo ilivyo kwa mtu kusom vitabu, kufumbua mafumbo au mazoezi mengine ya ubongo yanavyosaidia kuimarisha akili ya mtu.

Kula mlo kamili kunasaidia usipate maradhi ya mara kwa mara na kukupa afya bora lakini hakutakupa uwezo wa kukimbia kilometa 21 ndani ya saa moja au kukupa ‘six pack’ na ‘flat tummy’. Yapo mazoezi ya kukimbia ambayo yatausaidia mwili wako kuweza kufikia uwezo wa kukimbia km 21 ndani ya saa moja na pengine utahitaji kufanya mazoezi ya ‘abs’ na kuinua vyuma ili kupata six pack yako. Ubongo pia una mazoezi yake ili ufanye kazi vyema ikiwemo usomaji wa vitabu, kufumbua mafumbo mbalimbali yanayohitaji uchangamshe akili  pamoja na mazoezi mbalimbli ya ubongo.

Hivi ni baadhi ya vitabu vitakavyokusaidia kuimarisha akili yako;

“Tactical Thinking: 50 Brain-Training Puzzles to Change the Way You Think”

Kitabu hiki kilichoandikwa na Charles Phillips kina mafumbo “puzzles kutoka rahisi kabisa hadi ngumu zitakazosaidia kukufundisha lakini pia kukuza uwezo wa akili yako.

“Think Like a Freak: The Authors of Freakonomics Offer to Retrain Your Brain”

Waandishi maarufu wawili Steven Levitt na Stephen Dubner wamekuja na kitabu hiki ambacho kinakusaidia kubadili ufikiri wako. Ukweli ni kwamba mabadilikko yoyote unayotaka kufanya huanzia kichwani. Kitabu hiki kitamsaidia msomaji kuwa na fikra endelevu, kuwa mbunifu na kuwa na busara katika kufanya mambo na kutoa njia za kufuata ili kufanikisha hayo na kuwa na mafanikio yanayoweza kujulikana kimataifa.

“The Sherlock Holmes Puzzle Collection”

John Watson ameandika kitabu hiki kwa mfumo wa mafumbo yatakayochangamsha akili kufikiri ili kupata jibu sahihi, huku ukijifunza kuwa na subira katika kufikiri na kuchanganua majibu yako kabla ya kuyatamka.

“Your Brain at Work: Strategies for Overcoming Distraction, Regaining Focus, and Working Smarter All Day Long”

Ukitaka kuja kwanini kuna muda unaweza kuhisi kuwa akili imeelemewa sana na huwezi kufanya kitu basi kitabu cha David Rock ni sahihi kwako kusoma. Kinakupa mbinu za kutafuta utulivu, kufanya maamuzi bila majuto na kuwa na akili yenye afya.

“The Power of Habit: Why We Do What We Do in Life and Business”

Mbina za kukusaidia kuacha aina fulani ya tabia zinazokurudisha nyuma na kuiandaa akili yako kujenga mazoea mapya na mazuri zimeorodheshwa katika kitabu hiki kilichoandikwa na Charles Duhigg mwandishi mwenye kushinda tuzo mbalimbali ikiwemo Tuzo ya Pultizer inayotolewa kwa waandishi nchini Marekani.

“Train Your Brain for Success: Read Smarter, Remember More, and Break Your Own Records:

Roger Seip amekusanya mbinu mbalimbali zilizojaribiwa na kuthibitishwa kufanya kazi. Ni mbinu ndogo ambazo unaweza usidhani zinaweza kukusaidiaza, lakini hufanya kazi kwa ufanisi. Hata kama hufikirii kuwa kumbukumbu yako inahitaji kuboreshwa.

“Train Your Brain: 60 Days to a Better Brain”

Mwanasayansi wa Kijapani na mtaalamu wa sayansi ya neva za fahamu Ryuta Kawashima anakutembeza katika programu yake ya siku 60 itayosaidia kukuza “grey cells.” Hizi ni seli ambazo husaidia kwenye ufikiri na uhifadhi wa kumbukumbu kwenye ubongo.

“Unlimited Memory: How to Use Advanced Learning Strategies to Learn Faster, Remember More, and Be More Productive”

Kevin Horsley anakuonesha zana za kutumia, mikakati, na mbinu za kuboresha kumbukumbu yako. Kujifunza jinsi ya kufuatilia jambao kwa umakini, kuhifadhi na kukumbuka taarifa muhimu, na kutopoteza muda.

“It Doesn’t Have to Be Crazy at Work”

Kitabu hiki, kimeandikwa na waanzilishi wa ‘Basecamp’ Jason Fried na David Heinemeir Hansson ambao wananyambua kwa kina njia mpya ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili kujenga kile wanachorejelea kama “kampuni tulivu.”

Kwa pamoja wanakataa suala zima la kuwa ili kufanikiwa lazima utumie muda mrefu bila kulala wala mapumziko. Wanapendekeza utamaduni wa kampuni na uongozi unaounga mkono utulivu, uangalifu, na kujijali ili kupunguza machafuko na wasiwasi miongoni mwa watu na wafanyakazi wenzao.

Japo vitabu hivi ni vya lugha ya Kiingereza na pengine wengine wasiweze kuvisoma, ila umuhimu ni kujisomea vitabumbalimbali vyenye maudhui ya kukufanya ufikiri mambo chanya na kukufanya kukua kimaisha kwa lugha ambayo wewe unaielewa.

error: Content is protected !!