Shaka amtolea uvivu Mbatia

HomeKitaifa

Shaka amtolea uvivu Mbatia

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amemtaka Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kubadilika na kuanza kujadili siasa zenye manufaa ya kisera na utendaji bora badala ya kuzungumza kupatia au kukosea matamshi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, anapotaja takwimu.

Shaka alisema kwamba Mbatia inabidi afanye juhudi kukinusuru chama chake ili kiwe kinachojadili nguvu ya hoja na sio kufanya siasa za bei rahisi ili kisizidi kuporomoka kisiasa huku akisisitiza kuwa kupatia kutamka takwimu au kukosea hakuwezi kumsaidia mwananchi wa kawaida anayeishi vijijini lakini anapoonekana kiongozi kama Mbatia aking’angania jambo lisilo kuwa na msingi ni fedheha kwake na chama chake.

“Wananchi , wasomi na wenye maarifa wamekuwa wakisifu utawala wa Rais Samia, yakiwemo mataifa makubwa na taasisi za kimataifa. Mbatia aache siasa za jikoni, badala yake awe mkweli kwa yanayofanywa na utawala wa Rais Samia,” alisema Shaka.

Katibu Shaka aliwataka wananchi kupuuza yale yalisemwa na Mbatia huku akisisitiza kuwa uwezo wake wa kisiasa umegota ukingoni, kutokana na kushindwa kuwa na maarifa na ndiyo maana mara zote amekuwa akitoa matamshi yasiyokuwa na uzito wala maslahi mapana kwa taifa.

error: Content is protected !!