Majaliwa avunja ukimya kuelekea uchaguzi 2025

HomeKitaifa

Majaliwa avunja ukimya kuelekea uchaguzi 2025

Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa hana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2025 kama ambavyo inavumishwa kupitia mitandao ya kijamii. Waziri Majaliwa anasema kuwa watu hao wana nia ya kumchafua na kuvuruga utulivu na kasi ya maendeleo yanayopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu.

“Huo ni mkakati wa kuchafuana unaofanywa na baadhi ya vikundi vya watu wasiofahamu walitendalo. Hao ni wanaokwazwa na utendaji wangu wangu hivyo wanaona watumie njia hiyo ya kunichafua. Kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu, mimi wala sijawahi kuwa na mpango wa kugombea urais sijawahi kuwa na mpango huo kabisa. Mwaka 2025 mgombea wetu ni Rais Samia tu”.

Aidha, Waziri Mkuu alimshukuru Rais Samia kwa kumpa heshima ya kuwa msaidizi wake, na kusema kuwa siku zote kama msaidizi atatumika kwa niaba ya mkuu wake. Amesema “nafanya kazi kama Mtendaji Mkuu wa Serikali, nafuatilia maagizo,  maelekezo, usimamizi wa bajeti ya serikali, utendaji wa watumishi wa ngazi zote mpaka kijijini kwa kumsaidia Rais kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi, gharama halisi na fedha zinafanya kazi zilizokusudiwa bila kuchepushwa”.

 

Jamhuri

error: Content is protected !!