Zungu amuahidi Samia urais 2025

HomeKitaifa

Zungu amuahidi Samia urais 2025

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azan Zungu amemtaka Rais Samia Suluhu kutokuwa na wasiwasi kuhusu uchaguzi Mkuu ujao wa 2025, akisema wananchi wanampenda hivyo atapita na kuongoza kwa awamu nyingine.

“Usiwe na hofu kuhusu uchaguzi unaokuja 2025, wananchi wote wanakupenda. Hawawezi kukupenda wote lakini wengi wamekubali na kwa dua za vijana hawa na dua za masheikh na wachungaji wetu mambo yatakuwa mazuri,” alisema Zungu.

Zungu alikiri kwamb akitendo cha Rais Samia kwenda kuwatembelea wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Benjamini William Mkapa, jijini Dar es Salaam ni jambo jipya kwake kwani hakuna mtangulizi wake hata mmoja aliyewahi kufanya hivyo.

“Kwa mujibu wa historia ya nchi yetu hii ni mara ya kwanza Rais ambaye yuko katika madaraka anakutana na wanafunzi kama hawa leo, nilianza kazi zangu za siasa 2000, wakati Mzee Mkapa akiwa Rais hakufanya hivi, Jk hakufanya na hayati JPM hakufanya lakini wewe umefanya,” amesema Zungu.

error: Content is protected !!