Sirro aridhishwa na hali ya Loliondo

HomeKitaifa

Sirro aridhishwa na hali ya Loliondo

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya ziara katika eneo la Loliondo, Ngorongoro kwa ajili ya kujionea zoezi linaloendelea la uwekaji alama za mipaka, ambapo ameeleza kuridhishwa na kasi iliyopo.

IGP Sirro ambaye jana alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, aliwataka washiriki wa zoezi hilo kujituma ili kazi ya uwekaji alama za mipaka katika eneo hilo liishe kwa wakati.

Sirro alisisitiza wananchi kuwa watulivu na kushirikiana na serikali katika uamuzi huu wenye lengo la kuhifadhi eneo hilo kwa faida mtambuka za nchi.

“Msikubali kutumika kuchochea vurugu ambazo hazina manufaa kwa pande zote na wala msikubali kutumika kwa niaba ya wale wote wasiotutakia mema katika taifa,” alisema IGP Sirro.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alimhakikishia kuwa zoezi linaendeshwa kwa hali ya utulivu na kwa kuzingatia sheria za nchi.

error: Content is protected !!