Ziara ya Rais Samia India itakavyodumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano

HomeKitaifa

Ziara ya Rais Samia India itakavyodumisha, kuimarisha na kuendeleza uhusiano

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa January Makamba amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa na ziara nchini India kuanzia Oktoba 8 – 11 mwaka huu ikiwa ni baada ya miaka 8 tangu kiongozi wa mwisho wa Tanzania kutembelea nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Makamba amesema madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha, kudumisha na kuendeleza uhusiano baina ya Tanzania na India pamoja na kutafuta fursa za biashara na uwekezaji.

“Madhumuni ya ziara ni kuimarisha, kudumisha na kuendeleza uhusiano huo uliokuwepo kwa muda mrefu kati ya nchi zetu mbili hasa katika sekta za kimkakati viwanda, afya , elimu, biashara, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, sekta ya maji na sekta ya kilimo.” amesema Waziri Makamba.

India ni moja ya nchi ambazo ni vyanzo vikubwa vya uwekezaji hapa nchini na biashara katika ya Tanzania na India ni kubwa, hivyo basi ziara hii inaenda kudumisha huusiano uliodumu kwa miaka mingi.

error: Content is protected !!