Shuhuda aelezea Ofisa Mtendaji wa Kata alivyouawa ofisini Dar es Salaam

HomeKitaifa

Shuhuda aelezea Ofisa Mtendaji wa Kata alivyouawa ofisini Dar es Salaam

Ziana Mohammed, shuhuda wa mauaji ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mbezi Msumi, Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, Kelvin Mowo, amesema  alienda ofisi  ya kata kuchukua barua kwa ajili ya kwenda polisi kuripoti baada ya kuibiwa vito vya thamani nyumbani kwake, na kwamba akiwa anaendelea kuchukuliwa maelezo mtendaji huo alikatwa shingoni na panga.

Kabla tukio halijatendeka  vijana wanne walifika wakisubiri kuhudumiwa na mtendaji, lakini ghafla vijana hao wakaanza kulalamika mtendaji anawachelewesha, ndipo mtendaji akawaruhusu kuingia ofisini, lakini walisema kuna dada wanamsubiri, hivyo mtendaji akaendelea kumhudumia Zaina.

Shuhuda amesema mtendaji akampigia simu huyo dada na kumuweka loudspeaker, ndipo huyo dada akaomba apewe dakika 10 atakuwa amefika. Baada ya maongezi hayo ndipo tukio la mauaji lilitendeka.

“Baada ya tukio vijana watatu kati ya wale wanne walikimbia na yule aliyefanya tukio akawa anatoka nje polepole, niliendelea kupiga yowe lakini sababu nina presha nilijikuta nimepoteza fahamu.”

Kwa mujibu wa familia, Mowo ameacha mke ambaye ni mjamzito pamoja na mtoto mmoja.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro amesema watu watatu wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo wanahojiwa kwa kina na watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo huku majina ya watuhumiwa hao yakiwa yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi. #clickhabari

error: Content is protected !!