Waziri Makamba aeleza sababu ya kugawa mitungi ya gesi

HomeKitaifa

Waziri Makamba aeleza sababu ya kugawa mitungi ya gesi

Waizri wa Nishati, January Makamba amesema wizara hiyo imegawa bure mitungi ya gesi kwa kaya masikini na mamalishe katika mikoa mbalimbali nchini, ili kuiwezesha serikali kupata mrejesho wa matumizi sahihi ya gesi.

Lengo jingine ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto za kutumia kuni na mkaa kupikia, hali inayochangia madhara mbalimbali ikiwemo moshi unaosababisha maumivu ya kifua, kichomi na magonjwa ya upumuaji.

Waziri huyo yupo katika ziara kwenye mikoa 14 kuangalia shughuli zinazotekelezwa na taasisi zilizo chini ya wizara yake na kupokea maoni na kesro za wananchi.

Tayari Waziri Makamba ameshagawa mitungi zaidi ya 1,200 kwa kina mama na kaya masikini za mikoa ya Kagera, Simiyu, Mwanza na Mara, amekuwa akiwafuata mamalishe kwenye maeneo yao ya kazi ili kuhamasisha wengine kutumia nishati hiyo.

 

error: Content is protected !!