Fahamu madhara ya kukaa kwenye kiti muda mrefu

HomeElimu

Fahamu madhara ya kukaa kwenye kiti muda mrefu

Wafanyakazi wanaokaa kwenye viti muda mrefu ofisini, wapo hatarini kuvimba miguu kutokana na kubana mishipa ya damu.

Wanashauriwa kujenga tabia ya kusimama na kufanya mazoezi ya kunyoosha mwili ili kujiepusha kubana mishipa hiyo.

Mtaalamu wa udhibiti wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo, alisema wafanyakazi hususani Makatibu Mahsusi ambao wanakaa zaidi ya saa tatu wanapaswa kutenga muda kidogo wa kutembea ili kuipa nafasi mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.

“Kiafya sio vyema mtu kukaa chini ziaid ya saa tatu unapaswa kusimama na kutembea kidogo ili kuipa nafasi mishipa ya damu kufanya kazi yake vizuri ya kusambaza damu na kuepusha tatizo la kuvimba miguu,” alisema Dk. Nzobo.

Dk. Nzobo alisema, mazoezi ya kufanya sio kukimbia pekee, kutembea ni mazoezi mazuri hususani kwa mtu ambaye hajawahi kufanya mazoezi.

“Unaweza kuanza na mazoezi ya kutembea umbali mfupi na kadri siku zinavyozidi kwenda unaongeza umbali wa kutembea na mwili ukitoa jasho basi umefanya mazoezi ya kutosha,” alisema Dk. Nzobo.

 

error: Content is protected !!