Rais wa Bara la Afrika

HomeKitaifa

Rais wa Bara la Afrika

Katibu Mtendaji wa Eneo HUru la Biashara Afrika (AfFCTA), Wakele Mene amesema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa Rais Samia Suluhu Hassan si kiongozi wa Tanzania pekee bali wa Bara la Afrika kutokana na nidhamu ya uongozi bora inayotambulika na kuheshimika duniani.

Mene alisema dunia na bara la Afrika linaangalia aina ya uongozi wa Rais Samia na kwamba utendaji wake umekuwa wa mfano.

“Binafsi kila penye uongozi thabiti napenda kujifunza na ninapenda kuwa sehemu ya uongozi huo hivyo Watanzania mtambue kuwa Rais Samia sio wenu pekee yenu ni kiongozi wa Afrika,”alisema Mene.

Mene alisema washiriki kutoka mataifa mbalimbali wameshiriki maonesho hayo kwa sababu wana uhakika wa kufanya biashara na uwekezaji kwenye nchi iliyotulia, hivyo Watanzania nao wachangamkie fursa ya soko la Afrika.

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!