Sh8 bilioni zatengwa kusomesha madaktari

HomeKitaifa

Sh8 bilioni zatengwa kusomesha madaktari

Serikali imetenga Sh8 bilioni kwa ajili ya kusomesha madaktari na wataalamu ndani na nje ya nchi.

Imesema kati ya fedha hizo, Sh3 bilioni zitatumika kuwasomesha madaktari bingwa wa fani mbalimbali nje ya nchi na Sh5 bilioni zitawasomesha madaktari kwa ngazi ya uzamili, na nafasi hizo zinatarajiwa kutangazwa mapema Agosti, mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi baada ya kuwatembelea watoto (Rehema na Neema) walifanyiwa upasuaji wa kutenganishwa Julai Mosi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kueleza kuwa hapa nchini bado kuna changamoto ya wataalamu hasa wa upasuaji wa toto.

Makubi alisema taarifa alizozipata ni kuwa wataalamu wa upasuaji wa watoto wako wanne, watatu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na mmoja akitokea Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

 

error: Content is protected !!