Mgawo wa maji mbioni kuisha

HomeKitaifa

Mgawo wa maji mbioni kuisha

Wakazi wa wilaya ya Ilala, Kigamboni na Temeke wako mbioni kusahau mgawo wa maji baada ya Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla jana kuwasha pampu ya kusukuma maji kutoka kwenye visima vya maji Kimbiji na Mpela kuelekea kwenye tangi la kupokea na kusambaza maji.

Kuwashwa kwa pampu hiyo kutapunguza makali ya mgawo wa maji unaoendelea katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kwa wakazi wa Kigamboni na wilaya ya Ilala yote ikiwamo katikati ya jiji kuanzia Novemba Mosi.

Makalla alisema visima hivyo vinazalisha lita milioni 450 kwa saa na maji yanayozalishwa yanapelekwa kwenye tangi lenye uwezo wa kupokea lita milioni 15.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa maji uliopo, Makalla alielekeza DAWASA kuhakikisha wakandarasi wanafanya kazi usiku na mchana iliifikapo Jumanne, lita milioni 70 ziwe zimefika kwa wananchi.

Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja alisema mpaka sasa visima saba kati ya 12 vya Kimbiji na Mpela vimekamilika na vile ambavyo havijakamilika vipo hatua za mwisho.

error: Content is protected !!